MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA KILIMO CHA UMWAGILIAJ​I BONDE LA MPUNGA BUMBWISUDI

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya jingo la Ofisi ya  CCM, wakati alipofika Wilaya ya Magharibi kwa ajili ya kukagua matengenezo ya majengo ya Ofisi hiyo ya CCM iliyopo  wilayani hapo,  akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM, wakati alipofika Wilaya ya Magharibi kwa ajili ya kukagua matengenezo ya Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi Zanzibar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa mabonde ya Mpunga ya Bumbwisudi, Kadili Ali ( kulia), wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji wa Mpunga katika Bonde la Mpunga la Bumbwisudi lililopo eneo la Popo Jimbo la Dole Unguja mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi wa Mwera Misufini Mkoa wa mjini Magharibi, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal, alipofika wilayani hapo jana Mei 21 kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Mwera Misufini.
 9 na 10:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mwera Misufini baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya CCM ya Tawi la Misufini Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar .(Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR).

Comments