MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AWASILI UTURUKI KUMUWAKILISHA RAIS JAKAYA KIKWETE

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Msaidizi wa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Modest Mero, baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Ataturk jijini Istambul jana Mei 7, 2011. Makamu wa Rais yuko nchini Uturuki kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Matifa unahusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza kesho na kumalizika Mei 13, 2011. Katikati ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka. Picha kwa hisani ya Ofisi ya makamu wa rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Sundery baada ya Dkt. Bilal kuwasili mjini Istambul jana Mei 7, 2011.Kushoto ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal na baadhi ya viongozi alioongozana nao baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Ataturk, Istanbul jana Mei 7, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya nchi maskini. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa rais



Comments