MAKAMU WA RAIS DK BILAL AUNGURUMA ISTANBUL KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAENDELEO YA NCHI MASIKINI

 Makamu wa rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Maalim, walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini, unaoendelea Jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika  Mei 13 mwaka huu. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiingia kwenye Ukumbi wa Mkutano, wakati aliwasili kwenye ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi masikini Duniani. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu, jijini Istanbul Uturuki. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika chumba cha mkutano alipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajia kumalizika Mei 13 mwaka huu. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Anna Tibaijuka, akiwa na Waziri wa Ofisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyihaji Makame (katikati) na Mbunge wa Kigamboni, Dar es Salaam, Dkt. Faustine Ndugule, wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano wakati walipohudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Comments