MACHAFUKO SUDAN YALETA BONGO MICHUANO YA KAGAME

HALI ya machafuko nchini Sudan imepelekea michuiano ya soka Afrika Mashariki na kati maarufu kama 'Kombe la Kagame' iliyokuwa ipigwe juni 5 hadi 25 kuhamishiwa jijini dar es Salaam, Tanzania imefahamika.
Hii itakuwa mara ya pili mfululizo kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa michuanoinayoratibiwa CECAFA ambapo mwaka jana ilikuwa mwenyeji wa michuano ya Chalenji ambapo mwaka huku timu ya Tanzania bara ikitwaa ubingwa.
Katibu mkuu wa baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholaus Musonye amesema kuwa wamefikia uamuzi wa kuihamishia michuano hiyo nchini Tanzania kutokana na usalama uliopo.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni APR ya Rwanda ambapo mwaka huu Tanzania iwawakilishwa na Simba Sports Club.

Comments