MUDA WA MASHINDANO YA BLOG WAONGEZWA

Kutokana na maombi ya wengi ambayo tumeyapokea. Tumeongeza muda wa kupendekeza majina yatakaoshiriki katika mashindano yetu. Hivyo tarehe ya kutuma majina ya blog hizo umebadilishwa kutoka tarehe 31 May 2011 kwenda tarehe 10 June 2011.


Pia kutokana na blog mbalimbali zimepost hili shindano letu na tumeona kuna maswali ambayo hayana majibu kwenye comments zao. Na sisi kwa vile hatutaweza kupitia kila blog iliyopost maelezo na kuwaelewesha watu. Hapa nitaweka majibu ya maswali baadhi nimeona yameandika najua kuna mengi lakini hatujaweza kuyaona. Ila kama una swali usisite kututumia.
NB:Blog hii pia imependekezwa kushiriki shindano hili, nawashukuru wote endelea kuipigia kura.
Kwa taarifa zaidi tembelea http://www.tanzanianblogawards.com/.

Comments