KIPA WA MTIBWA SUGAR SHABAN KADO ASAINI MIAKA MIWILI YANGA

MABINGWA wa ligi kuu bara timu ya soka ya Yanga kwa mara nyingine imeipiga bao la kisigino mahasimu wao nchini Simba baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa iliyekuwa ikimuwania, Shaban Hassan Kado wa Mtibwa Sugar.
Awali Yanga iliipiga Simba bao la kisigino kwa kiungo wa Ghana Kenneth Assamo ambaye ilitangaza kufanya mazungumzo na klabu yake, kabla ya Yanga kumleta nchini Assamoh na kumsainisha mkataba.

Comments