KINDAI SHOOTING WAVULIWA UBINGWA KILI TAIFA CUP

MABINGWA watetezi wa michuano ya kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup'imevuliwa ubingwa rasmi baada ya kufungwa mabao 3-0  na timu ya mkoa wa Ilala  katika mechi ya robo fainali iliyopigewa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Aidha, wenyeji wa fainali hizo Arusha nao wameaga michuano hiyo baada ya kubanjuliwa mabao 2-1 na Mwanza.
Kwa mantiki hiyo Ilala  na Mwanza watakutana katika nusu fainali.


Wachezaji wa timu ya mkoa wa Singida na Mkoa wa Ilala wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robofainali ya kwanza ya michuano ya Kili Taifa inayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Ilala ilishinda 3-0 na kuivua Singida ubingwa.

 Mchezaji wa timu ya Singida, Msengi Selemani (kushoto) na Ambatus Nesta wakiwania mpira wakati wa Robofainali ya kwanza ya michuano ya Kili Taifa Cup ianyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Ilala ilishinda 3-0 na kuivua Singida ubingwa.
Mchezaji wa timu ya mkoa wa Singida, Yahaya Ramadhani akimweka chini mchezaji wa timu ya mkoa wa Ilala, Erick Mawala wakati wa Robofaianali ya kwanza ya Michuano ya KiliTaifa Cup inayofanyika jijini Arusha. Ilala ilishinda 3-0 na kuivua Singida ubingwa.

Comments

  1. Mechi hizi ni nzuri kupata wachezaji, lakini kuna maoni kuwa mechi za kombe hili ziwahusishe `chipukizi' na wazawa wa mikoa husika...ili kupata wachezaji wengine...ambao hawapati nafasi kama hizi lakini wakipata wanaweza wakawa `STAR'

    ReplyDelete

Post a Comment