KINDA LA YANGA AWACHANA WACHEZAJI WA ZAMANI

CHIPUKIZI wa timu ya soka ya Yanga anaekipoiga katika timu ya Taifa ya vijana wwenye umri chini ya miaka 23 (U-23) Salum Telela (Pichani kushoto)amesema wachezaji wa zamani walikuwa hawajityumi kama ilivyo wa sasa.
Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo maana miaka ya nyuma hakukuwa na wachezaji wengi wa Tanzania waliokuwa wanapata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa.
"Wachezaji wa zamani walikuwa hawajitumi kabisa...waliliridhika na hali ya kucheza hapa nchini...sasa hivi tunajituma sana ndiyo maana unaona kila kukicha baadhi yetu wanakwenda kufanya majaribio huku wengine wakisajiliwa katika timu mbalimbali barani Ulaya",

Comments