KANDORO, MWAKIPESILE WATAMBIANA KILI TAIFA CUP 2011

IKIWA imebaki siku moja bingwa ya mashindano ya Kili Taifa Cup 2011 kujulikana, Wakuu wa Mikoa ya Mwanza na Mbeya iliyoingia fainali wametambiana kila mmoja kuibuka na ushindi katika mechi ya kesho.
Timu za Mwanza na Mbeya zinashuka dimbani kesho Jumamosi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wakuu hao wa mikoa, kila mmoja alitamba kuondoka na kombe kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro alitoa pongezi kwa timu ya Mkoa wa Mwanza kwa kuuwakilisha mkoa huo vizuri na hatimaye kutinga fainali za KIli Taifa Cup.
Alisema ana uhakika kombe hilo litaenda Mwanza kwa kuwa wachezaji wa timu hiyo wana ari kubwa ya kushinda na wamejiandaa vizuri katika mechi ya kesho.
Alisema yeye binafsi hataweza kufika Arusha kushihudia mechi hiyo kwa kuwa ana majukumu mengine lakini atawatuma wawakilishi ili waungane na viongozi wa timu hiyo kuipa nguvu imu ili ishinde.
"Mimi nitakuwa na majukumu mengine lakini kuna watu wataenda kuungana na viongozi wetu katika kuwapa nguvu vijana...tuna matuimani makubwa ya kombe hilo kuja Mwanza,"alisema Kandoro.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile,ameipongeza timu yake kwa kufika hatua hiyo ya fainali ya michuano hiyo.
Mwakipesile alisema yeye atakuwa mkoani Arusha kuipa nguvu timu yake ambayo ana uhakika itanyakuwa ubingwa huo.
Mwakipesile alisema kabla ya yeye kuja ametuma ujumbe wa viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya, pamoja na Mkuu wa Wilaya Mbeya na Meya ya Jiji la Mbeya.
"Mimi nitakuja siku ya mechi lakini jana nimeshatuma watu waweze kuipa nguvu zaidi...ubingwa wa mwaka huu hauna ubishi ni wetu tutalichukua kombe na kwenda Nalo Mbeya,"alisema Mwakipesile.
Alisema kuwa Mkoa wa Mbeya ulisisimka mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo hivyo macho na masikio ya wakazi wa mbeya yapo mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuiombea timu yao iweze kufanya vizuri zaidi.
Waliluokuwa mabingwa watetezi, Singida tayari walishayaaga mashindano haya baada ya kufungwa magoli matatu na Ilala katika hatua ya robo fainali.
Katika hatua nyingine, wachezaji wa timu hizo mbili, Gaudence Mwaikimba na Jerryson Tegete wanawania kuwa wafungaji bora wa mashindano kwani ndio wanaongoza mpaka sasa. Mwaikimba ana magoli saba na Tegete ana magoli sita hadi mechi za juzi.
Mfungaji bora wa mashindano anatarajiwa kupata Tsh milioni mbili.
Leo ni zamu ya Ilala na Kagera ambao watachuana ili kumpata mshindi wa tatu katika mashindano haya. Mechi hiyo itachezwa saa tisa na nusu adhuhuri.
Mechi ya kesho ya fainali inatarajiwa kuanza saa tisa na nusu adhuhuri katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid na kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maandalizi yote yamekamilika.
Mshindi atapata kitita cha shilingi milioni 40, mshindi wa pili milinoi 20 na wa tatu milioni 10.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solutions.
Michael Mukunza
Media Manager
Executive Solutions Ltd
P.O. Box 1601, Dar es Salaam
Mobile: 0784/0776/0767978302 or 0714683451

Comments

Post a Comment