ILALA YASHIKA NAFASI YA TATU KILI TAIFA CUP 2011


 Mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Kagera, Ananius Kaijage (kushoto) akichuana na beki wa timu ya mkoa wa Ilala, Amandus Nesta wakati wa mchezo wa kutafuta msindi wa tatu wa michuano ya Kill Taifa Cup 2011 uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Beki wa timu ya Mkoa wa Ilala, Ramadhani Kauga (kushoto) akimzuia mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Kagera, Jumja Hamis Nade, wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Kill Taifa Cup 2011 uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

TIMU ya Mkoa wa Ilala imenyakua nafasi ya  tatu wa michuano ya Kili Taifa Cup baada ya kuifunga timu ya Mkoa wa Kagera kwa mabao 2-1,mchezo uliopigwa  jioni ya leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Goli la kwanza la Ilala lilipatikana dakika ya 25 ya mchezo lililofungwa na Vedastus Foto kwa njia ya penati baada ya beki wa Kagera Abuu Balekao kumuangusha katika eneo la hatari Omary Matuta ndipo mwanmuzi wa mchezo Israel Nkongo alipoamuru ipigwe penati
Dakika ya 42 ya mchezo Shamte Odiro aliipatia timu yake goli la kusawazisha baada ya kutokea patashika ya piga nikupe langoni mwa timu ya Ilala.
Dakika ya 47 ya mchezo Ilala kupitia kwa mchezaji wake Samwel Rogart ilipata goli la pili baada ya kupiga shuti la mbali lililotinga moja kwa moja wavuni.
Mchezaji bora wa mchezo huo ni Samweli Rogert amejinyakulia kitita cha laki moja na Ilala imejinyakulia milioni 10 kwa kushika nafasi hiyo.
Fainali ya michuano hiyo itafanyika kesho ambapo Mwanza itakwaana na Mbeya.

Comments