ILALA V MWANZA KUKWAANA KESHO KATIKA NUSU FAINALI KILI TAIFA CUP

TIMU ya soka ya Mkoa wa Ilala na Mwanza kesho zina kibarua kigumu kwani zinakutana katika hatua ya Nusu fainali ya kwanza ya michuno ya Kili Taifa Cup inayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani hapa.
Kindumbwendumbwe hicho kitaanza saa 10.00 Alasiri ambapo mshindi wa mchezo huo atamsumbiri mshindi wa michezo wa keshokutwa wa hatua hiyo kwa ajili ya kucheza fainali siku ya Jumamosi.
Endapo dakika 90 za mchezo zitamalizika bila ya kupatikana mshindi timu hizo zitapiga penati tano tano ambazo zitatoa mshindi na atakayetolewa atacheza hatua ya kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Ijumaa.
Mchezo wa leo unaatabiriwa kuwa mkali na wanguvu kutokana na timu hizo kuwa na uwezo mkubwa katika kusakata kabumbu.

Ilala yenye wachezaji waliowahi kuwika katika Ligi kuu kama vile Salum Mpakala, Adam Kingwande Omar Matuta na Anthony Matangalu,katika misumi kadhaa wanaweza wakawanaweza wakawa mwiba mkali kwa timu ya Mwanza iliyona mchezaji wa Yanga Jerry Tegete.
Bingwa wa Michuano hiyo atanyakuwa kitita cha Sh.milioni 40, mshindi wa pili Sh.milioni 20 wakati wa tatu sh.milioni 10.

Comments