FAIDA YA KUJITIBU NA KITUNGUU MAJI

Kitunguumaji ni aina ya mboga ya yungiyungi. Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha. Anaeikitumia kitunguu maji ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwasababu hufanya oksaidi (oxide) na huwa kiini chenye sumu. Kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa fresh.

Imethibitiswa kisayansi kuwa juisi yake huuwa vijidudu vya kinamasi na vya kifua-kikuu, huuwa baada tu ya kunusa moshi wake.
Nchi mashuhuri duniani katika upandaji wa kitunguumaji ni Misri (Egypt). Razi amesema: "Kitunguu maji kikifanyiwa achari, ukali wake hupungua na hutia nguvu maida, na kitunguu kilichofanywa achari, hufungua mno hamu ya kula" Kwa ajili hiyo watu wa misri hula ktunguumaji kikiwa kimechomwa, hutia nguvu mwilini, huufanya uso kuwa mwekundu na huimarisha misuli.
Ibn Baitar amesema: " Kitunguu maji hufungua hamu ya kula, hulainisha tumbo. Kikipikwa hukojoza na huzidisha nguvu za kiume kikichemshwa. Na kinachokata harufu ya kitunguumaji ni lozi (almond).ntaky amesema kuhusu kitunguu maji: "Hufungua vizuizi mwilini, hutia nguvu za shahawakwa mwanamke na mwanaume mbili (ya kula na na kujamii) hasa kikipikwa kwa nyama, pia huondoa homa manjano (jaundice) hukojoza na kumimina hedhi pamoja na kuvunja vijiwe tumboni".
Katika gazeti moja huko Ufaransa liitwalo "Everything" (Kila kitu) limeelezea kuwa daktari mmoja aliwatibu wagonjwa kwa kuwapiga sindano (ya kitunguumaji) wagonjwa wengi waliokuwa na saratani (cancer) na akapata matokea mazuri.
Viini vyenye athari nzuri katika kitunguu maji ni Vitamin C (antiseptic) inayozuia kukua kwa bakteria (bacteria) kwenye jeraha, ngozi n.k pia hutia nishati homoni (hormones) wa nguvu za kiume, kiini cha insulini (insuline, itumikayo kutibu wagonjwa wa kisukari). Kwa hivyo kitunguu maji ni katika dawa yenye kuwatibu wagonjwa wa kisukari, ndani yake mnapatikana salfa, chuma na vitamini zinazotia nguvu mishipa. Vilevile hupatikana viini vyenye kukojoza, kutoa safura na vyenye kutia nishati moyo pamoja na mzunguko wa damu mwilini.
Pia imethibitishwa kuwa katika kitunguu maji muna vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini (penicillin) kwahivyo hupoza kifua kikuu, kaswende (syphillis) na kisonono (gonorrhea), na huua aina ya vijidudu vingi vya hatari.
Pamoja na kuwa tunaamini kuwa maisha ya mwanaadam yote yamo katika mikono ya Allah S.W, lakini imethibitishwa kuwa wale watumiaji wa vitunguu maji zaidi huwa na umri mrefu pia huepukana na maradhi ya saratani na kifua kikuu. Mwandishi wa kitabu cha tiba zinazotokana na kitunguu maji yeye amekiita kitunguu maji ni " mpira wa dhahabu" kwakuwa ndani yake muna manufaa mengi yenye utajiri wa afya. Kutakasika ni kwa Allah mwenye kuneemesha peke yake.
NIMETUMIWA NA JAMES BIBOZE

Comments

  1. Duh, ndugu yangu hili darasa safi sana, nashukuru, kumbe vitu asilia ni dawa...TUPO PAMOJA

    ReplyDelete

Post a Comment