CANNAVARO AIKANA SIMBA, YANGA YAMUONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI

BEKI wa timu ya soka ya Yanga  Nadir Haroub 'Cannavaro' (pichani kushoto)amekana kusaini mkataba wa kuichezea klkabu ya soka ya Simba katika msimu ujao wa Ligi na Michuano ya Kimataifa.
Cannavaro ambaye amebakiza mkataba mmoja ndani ya Yanga,amekiri kuwa ni kweli  viongozi wa Simba wamekuwa wakimtaka kwa udi na uvumba ikiwemo kumshawishi kwa fedha lakini hakuwa tayari kuisaliti timu yake hiyo bingwa wa ligi kuu bara.
hata hivyo, tayari Yanga imemuongeza mkataba mwingine beki huyo baada ya jana kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo.
Kwa mantiki hiyo, Cannavaro anamkataba wa miaka mitatu hivyo ataitumikia yanga hadi msimu wa 2014/2015.

Comments