MBEYA v MWANZA SASA FAINALI KILI TAIFA CUP 2011

Beki wa timu ya mkoa wa Mbeya, David Mwantika (kushoto) akimzuia mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Kagera, Fikiri Omary wakati wa mchezo wa nusu faianli ya pili ya michuano ya Kill Taifa Cup 2011 uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha leo.
Mchezaji wa timu ya mkoa wa Mbeya , Benjamin Asukile akiondoa hatari wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya michuano ya Kill Taifa Cup 2011 dhidi ya timu ya mkoa wa Kagera uliofanyika katika Uwanaja wa Sheikh Amri Abeid Arusha leo.

Kipa wa timu ya mkoa wa Kagera akiruka bila mafanikio baada ya penalti iliyopigwa na mshambuliaji wa timu ya mkoa wa mbeya, Gaudens Mwaikimba baada ya kipa huyo kumfanyia madhambi mchezaji wa timu ya Mbeya katika eneo la hatari

TIMU ya Mkoa wa Mbeya itakwaana na Mwanza katika mcezo wa fainali za michuano ya kombe la Taifa 'Kili taifa Cup[' utakaopigwa jumamososi katika dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Mbeya  imeingia hatua ya Fainali baada ya kuifunga timu ya Mkoa wa Kagera kwa mabao 2-1,mchezo uliyofanyika kwenye Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Goli la lilipatikana dakika ya 24 ya mchezo lililofungwa na Gaudence Mwaikimba baada ya kipa wa Kagera kumkwatua mchezaji Said Mtupa,eneo la hatari.
Dakika ya 60 Themi Felix, aliipatia  Kagera goli la kusawazisha baada ya kutokea patashika langoni mwa Mbeya ambapo kipa wa Mbeya aliudaka mpira na kumponyoka kumfika miguu mwa mfungaji.
Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka kwa goli 1-1 ndipo zilipoongezwa dakika na dakika ya 93 ya mchezo beki wa timu ya Kagera alijifunga akiwa katika harakati ya kuokoa ndipo mpira uliponasa wavuni.
Mpaka dakika 120 zimelizika Mbeya imeungana na Mwanza kucheza hatua ya fainali ambayo itachezwa Jumamosi na mchezo wa kutafuta mshindi watatu utafanyika Ijumaa, ambapo Ilala itakipiga na Kagera kuwania nafasi hiyo.
Mchezaji Bora katika mchezo huo alikuwa George Charles,aliyejinyakulia kitita cha sh.100,000 kutoka kwa wadhamini wa michuanohiyo Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinyaji chake Kilimanjaro.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habari yanaratibiwa na kampuni ya Executive Solution.

Comments