BIRMINGHAM YARIDHISHWA NA MIUNDO MBINU YA TZ KUJA JULAI KAMA KAWAIDA

MABINGWA wa kombe la Carling timu ya Birmingham ya nchini Uingereza imeridhishwa na miundombinu iliyopo nchini Tanzania na hivyo kuridhia kuja mwezi Julai mwaka huu kwa ziara ya kimichezo.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Rage ambao watakuwa wenyeji wa timu hiyo amesema kwamba kupitia ukaguzi wa hospitali, hoteli, Uwanja na huduma nyingine walizofanya viongozi wa timu hiyo akiwemo Daktari Ian Mc GUINNESS na Kocha msaidizi wa timu hiyo Andy Watson juzi ni wazi kuwa sasa ujio wa timu hiyo utakuwa kama ilivyopangwa awali.
Pindi itakapokuja nchini timu hiyo itakipiga na Simba usiku wa Julai saba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kukipiga na Yanga Julai 11 katika Uwanja huo.
Aidha, wakali hao wanatarajiwa kuja nchini na ujumbe wa watu zaidi ya 1000 ambao watajigharamia wenyewe kila kitu.

Comments