ARUSHA LAZIMA TUTWAE UBINGWA WA KILI TAIFA CUP-ALDINA

KIPA wa timu ya mkoa wa Arusha 'Mount Meru Worriors'Alidina Hashim (pichani kushoto)amejitapa ya kuwa ni lazima timu yao itwae ubingwa wa michuano ya kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup' kwa mwaka huu.
kipa huyo amesema anauhakika na hilo kutokana na ubora wa timu yake pamioja na maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa muda mrefu.
Akizungumza mjini Moshi hivi karibuni katika hatua ya awali ya michuano hiyo ambapo timu yao ilikuwa katika kituo hicho kipa huyo alisema itakuwa ni jambo la ajabu kwa wenyeji wa fainali hizo (Arusha) kushindwa kunyakua ubingwa.
"PAmoja na uenyeji hata hali ya hewa ya huku tumeizoea, itakuwa ni aibu sana sisi kama wenyeji tukishindwa kuutumia vema uwanja wetu wa nyumbani", Alisema.
Robo fainali ya michuano hiyo imepangwa kuanza mei 21 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha huku, fainali za michuano hiyo zikifikia tamati mei 28

Comments