YANGA KUWAADHIBU NURDIN, CANNAVARO

NURDIN BAKARI
NADIR HAROUB 'CANNAVARO'

YANGA huenda ikawaadhibu nyota wake wawili Nadir Haroub 'Cannavaro' na Nurdin Bakari kutokana na kuzungumza sana na vyombo vya habari,imefahamika.
Mmoja ya viongozi wa klabu hiyo alisema jana kwamba wachezaji hao wanafanya hivyo wakati wakijua ni kinyume na taratibu za wachezaji wa klabu hiyo.
Alisema uongozi umekuwa ukichukizwa na tabia za wachezaji hao, kwani ni utovu wa nidhamu na kama wataendelea nayo watawachukulia hatua kali.
Hivi karibuni Simba pia iliwaadhibu wachezaji wake Mussa Mgosi kwa tabia kama hiyo na Kelvin Yondan ambaye alitoroka kambini.

Comments