WAJUMBE TFF WAICHANGIA STARS 1,980,000


MKUTANO MKUU WACHANGIA STARS

Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo inashiriki michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazochezwa Gabon- Equatorial Guinea mwakani imechangiwa sh. 1,980,000. Fedha hizo kwa Taifa Stars iliyo kundi D pamoja na Morocco, Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati zilichangwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika Machi 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Mkutano huo walishuhudia mechi kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyochezwa Machi 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Walichanga fedha hizo kuipongeza Stars baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.


MAPATO SIMBA v KAGERA SUGAR

Mechi namba 122 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera Sugar iliyochezwa Machi 29 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeingiza sh. 23,637,000. Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 3,605,644 fedha iliyobaki kwa mgawanyo kwa pande zote husika ni sh. 20,031,355.93. Jumla ya gharama za awali za mchezo ni sh. 3,635,600 wakati kila timu ilipata sh. 4,918,726.78. Uwanja sh. 1,639,575.59, TFF sh. 1,639,575.59, gharama za mchezo sh. 1,639,575.59, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 163,957.56, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 655,830.24 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 819,787.80. Boniface Wambura Ofisa Habari

Comments