WADAU WAITAKA TAMISEMI KUWAWEZESHA MAAFISA UTAMADUNI

AfisaUtamaduni wa Wilaya ya Ilala Bi.Shani Kitogo (Kulia) akisisitiza jambo wakatiakiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)linalofanyika kila Jumatatu.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.GhoncheMaterego.
Wakongwewakichangia mada kwa nguvu zote kwenye Jukwaa la Sanaa-Waziri Ally kutoka Kundi la Muziki la Kilimanjaro 'Wananjenje'


Na Mwandishi Wetu

Wadau wa Sanaa wameiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwawezesha maafisa utamaduni ilikusukuma shughuli za sanaa na utamaduni katika ngazi za wilaya na mikoa.


Wakizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kilaJumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wadau hao walisemakwamba,maafisa utamaduni wamekuwa wakipewa bajeti ndogo kiasi cha kufanyashughuli za sanaa na utamaduni kushindwa kuendelea na kukwama kabisa.


Aidha, walilalamikia hali ya Maafisa Utamaduni kuwa chini yaIdara ya Elimu na Mafunzo iliyo chini ya Afisa Elimu wa wilaya hali ambayoimewafanya wakose gawio la kutosha la bajeti kwa ajili ya maendeleo ya sekta yautamaduni badala ya wao kuwa na bajeti maalum kwa ajili ya kushughulikia sektahiyo muhimu.


“Maafisa Utamaduni wamekuwa wakipewa fedha kidogo sana,hataofisi zao hazieleweki kwani zimefichwa ndani ya idara ya elimu namafunzo ya wilaya.Wamekuwawakikumbukwa nyakati za Mwenge tu kwa kupewa fedha za kukamilishashughuli hiyo.


Kwahali hii sekta ya utamaduni itapiga hatua kweli?” alihoji NKwama Bhallangaambaye ni Mjumbe wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho nchini.Alizidi kueleza kwamba,sekta ya sanaa imekuwa ikishughulikiwana wizara tatu tofauti akimaanisha ya Viwanda na Masoko,TAMISEMI na ile yaHabari,Vijana,Utamaduni na Michezo hali ambayo imekuwa ikisababisha migonganoya kiutendaji na ukosefu wa usimamizi wa moja kwa moja wa sekta hii katikawizara moja.


Awali Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisemakwamba,kumekuwa na changamoto nyingi katika kuwafikia wasanii waliokowilayani nahata kusukuma maendeleo ya sekta ya utamaduni kwani maafisa utamaduni wamekuwachini ya idara elimu na mafunzo ambapo wamekuwa wakipata fedha ndogo sana kwaajili ya shughuli zao.


“Fedha za usajili wa wasanii mathalan, inabidi zirudi kwawasanii walioko wilayani lakini inakuwa ngumu kwa sababu maafisa utamaduni wakochini ya Afisa Elimu hivyo fedha hazitaweza kugharamikia sanaa bali shughulizingine tofauti.Hii ndiyo changamoto iliyopo na inapaswa kutatuliwa.


Aliongeza kwamba,BASATA limeshatuma waraka maalum kwawakurugenzi wa wilaya kuomba kuwe na akaunti maalum ya sanaa ili fedhazitakazotumwa ziwe zinatumika kwa wasanii na sekta ya sanaa pekee lakini hadisasa hilo halijafanyika.


Katika Jukwaa hilo la sanaa,Afisa Utamaduni wa Wilaya yaIlala Bi.Shani A. Kitogo aliwasilisha mada juu ya Ugharamiaji na uendeshaji washughuli za sanaa na Utamaduni katika ngazi ya Wilaya ambapo aliibua changamotombalimbali ikiwa ni pamoja na hiyo ya maafisa utamaduni kutokuwezeshwa.

Comments