WACHEZAJI TAIFA STARS MARUFUKU KILI TAIFA CUP


WACHEZAJI waliopo katika timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ hawataruhusiwa kushiriki michuano ya kombe la Taifa ‘Kili Taifa Cup’ mwaka huu.


Hayo yalisemwa na Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika semina ya waandishi wa habari za michezo iliyofanyika juzi kwenye hoteli ya South Beach, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.


Alisema lengo la mashindano hayo ni kuvumbua na kuinua vipaji vvya wachezaji toka mikoa mbalimbali nchini ambao baadaye wataweza kuwa wachezaji wazuri katika timu kubwa zikiwemo zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.


“hii ni michuano ya kuvumbua vipaji vipya pia kuendeleza vilivyopo, sasa kama utaweka wachezaji wa timu ya Taifa au wale wanaochezea timu za ligi kuu utapoteza maana ya michuano hii”, alisema.


Pamoja na timu kuzuiwa kusajili wachezaji wa timu ya Taifa, pia zimetakiwa kusajili wachezaji watano gtu wanaochezxea timu zinazoshiriki ligi kuu bara.


Hatua za mtoa za michuano hiyo zitapigwa katika kanda sita za Kilimanjaro, Mwanza, Tabora, Mbeya, Morogoro na Lindi huku kila kanda ikiwa na timu nje, kabla ya hatua ya robo fainali mpaka fainali kutimua vumbi mkoani Arusha.


Wadhamini wa michuano hiyo, kampuni ya bia Tanzania (TBL),kupitia bia ya Kilimanjaro chini ya uratibu wa kampuni ya Executive Solutions, wamepanga kutumia bil.1.3 ili kukamilisha michuano hiyo ambapo bingwa atapata mil.40, mshindi wa pili atapata mil.20 na mshindi wa tatu atapata mil.10.

Comments