U-23 YAPANGWA NA NIGERIA, WAJAZWA MIL.22




TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka U-23 imepangiwa kucheza na Nigeria katika raundi ya pili ya michuano ya Olimpiki ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Juni 4 na 5 mwaka huu.


Aidha, timu hiyo imekabidhiwa jumla ya sh. milioni 22 ambazo iliahidiwa endapo ingeitoa Cameroon kwenye michuano ya Olimpiki.


Fedha hizo ziliahidiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Simba Trailers. NSSF kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Dk. Ramadhan Dau ilikabidhi sh. milioni 10 wakati Azim Dewji ambaye ni Mkurugenzi wa Simba Trailers alikabidhi sh. milioni 12.


Kati ya fedha hizo ilizotoa Simba Trailers, sh. milioni 10 ni kwa ajili ya timu, sh. milioni mbili kwa ajili ya kipa aliyeokoa penalti na wafungaji wa mabao mawili ya U23.

Comments