U-23 YA TANZANIA YALALA 2-1 KWA VIJANA WA UGANDA 'THE KOBS'


TIMU ya soka ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 imetandikwa mabao 2-1 na vijana wenzao wa ugnda 'The Kobs' kupitia mechi ya awali ya kuwania kufuzu fainali za 'All Africa Games' .

Mechi hiyo ilipigwa katika uwanja wa Mandela (Namboole) Kampala, Uganda ambapo mabao ya The Kobs yaliwekwa kimiani na Moses Olaya (dk. 4) baada ya shuti lililopigwa na mshambuliaji Owen kasule kumtoka kipa Shabani Kado. Kiiza Hamis alifunga la pili (dk. 23) akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto. Bao la Tanzania U23 limefungwa dakika ya 46 kwa shuti la mbali (katikati ya uwanja) na Kigi Makasi.

Kocha wa U-23 Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema ameyapokea matokeo, hivyo atajipanga kwa mechi ya marudiano kwa kuufanyia kazi upungufu wote uliojitokeza katika pambano hilo.

Hata hivyo amekiri kuwa Uganda ni wazuri na anatambua kuwa watajipanga vizuri zaidi kwa mechi ya marudiano. U23: Shaaban Kado, Juma Abdul, Kigi Makasi, Babu Ally, Shomari Kapombe, Salum Telela, Mrisho Ngasa, Jabir Aziz, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata na Khamis Mcha/Awadh Juma. The Kobs: Benjamin Ochan, Saka Mpiima, Godfrey Walusimbi, Ivan Bukenya, Isaac Isinde, Kiiza Hamisi, Sadam Mussa, Moses Olaya/Siraje Turyamuhebwa, Owen Kasule, Emmanuel Okwi/Moses Kaye na Mike Mutyaba/Brian Majwega. U23 itarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu saa 8 mchana kwa ndege ya Air Uganda

Comments