TWIGA STARS YAFUZU 'ALL AFRICA GAMES'


TIMU ya soka ya Taifa ya wanawake 'Twiga Stars' imefuzu kucheza fainali za michezo ya Afrika 'All Africa Games' inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3-18, huko Maputo, Msumbiji.

Twiga Stars ilikuwa iiumane na Sudan katika mchezo wa mchujo Aprili 30 huko Khartoum, Sudan, lakini waponzani hao wamejitoa katika mchakato huo.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amesema wamepokea taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuhusiana na kujitoa huko.

Comments