TP MAZEMBE WATUA, WAGOMEA USAFIRI, HOTELI

MABINGWA wa ligi ya klabu bingwa ya Afrika Tp MAzembe ya Congo wamewasili jioni ya jana kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya ligi hiyo dhidi ya mabingwa wa TAnzania Simba ya Dar es Salaam itakayopigwa kesho kwenye Uwa nja wa Taifa. Hata hivyo, msafara wa watu 32 uliotua kwa ndege maalum uligoma kupanda magari waliyopandaliwa na wenyeji wao (Simba) na kisha kupanda usafiri walikuwa wameandaliwa na mashabiki wao wa huku. Kama hiyo haitoshi, Wacongoman hao waligoma kwenmda katika hoteli waliyoandaliwa na Simba (Durban) na kwenda kulala Movenpick.

Comments