SIMBA YAZIDI KUUWEKA REHANI UBINGWA


MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba wamezidi kuuweka rehani ubingwa wao baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 na maafande wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Jkt ilianza kuandika bao kupitia kwa mshambuliaji wake Hussein Bunu, huku bao la kusawazisha likiwekwa kimiani na Emmanuel Okwi kwa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 46 na mechi moja mkononi, hivyo kuuweka ubingwa wake rehani kwa Yanga yenye pointi 43 na mechi mbili mkononi, ambapo kesho inashuka dimba la Uhuru kuumana na African Lyon.

Endapo Simba itashinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Majimaji itafikisha pointi 49 na Yanga ikishinda mechi zake zilizosalia nayo itafikisha pointi 49 hivyo kuangaliwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Comments