SIMBA YAMUUZA DOLA 150,000 MBWANA SAMATA KWA TP MAZEMBE YA CONGO

MBWANA SAMATHA

KLABU ya soka ya Simba imemuuza kwa dola 150,000 sawa na shilingi mil.225 za Kitanzania mshambuliaji wake chipukizi Mbwana Samatha.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema katika fedha hizo , klabu itapa dola 100,000, wakati Samata atapata dola 50,000 kama ada ya uhamisho.

Rage ameongeza kuwa fedha hizo zitatumika kusajilia wachezaji kadhaa ambao wataitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Comments