NGUMI KURINDIMA PANANDI PANANDI LEO


MABONDIA wa ngumi za ridhaa wa mkoa wa Ilala wanatarajia kupanda
ulingoni leo katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Dar es Salaam.
ambapo kutakuwa na ngumi kutoka kwa mabondia mbalimbali toka pande
zote za mkoa wa DAr es Salaam

Tamasha hilo litakalokuwa likitimua vumbi kila wiki inatarajia
kuwakutanisha mabondia wa Ilala na wa sehemu nyingine za Dar es Salaam
ili kuweza kujipima nguvu katika kuinua mchezo huo katika mkoa huo.

Katika Tamasha hilo kesho bondia Mbwana Matumla anayejiaandaa kwa
ajili ya kushiriki katika kuwania ubingwa wa UBO pambano linalotarajia
kufanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa PTA dhidi ya Mkenya
Gabriel Ochieng atachuana na mabonmdia Yohana Robert na Issa Sewa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Tamasha hilo kupitia Taasisi
ya Kinyogoli foundation, Habibu Kinyogoli alisema mapambano yote
yatakuwa katika raundi nne huku pambano la Mbwana likiwa katika uzito
wa Kg 55 likiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano lake hilo.

Alisema, mkakati huo wa kuanzisha Tamasha akishirikiana na kocha
msaidizi wa timu ya mkoa huo Rajabu Mhamila 'Super D' utasaidia kuinua
vipaji vipya vya mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani kutawajenga
wachezaji kujikita katika mchezo huo na kuufanya kama ndio ajira yao.

Alisema, katika kulifanikisha hilo anawaomba wadau mbalimbali
kuwasaidia kuwadhamini ili waweze kufikia malengo yao katika kuinua
vipaji hivyo.pia alisema kutakuwa na wageni waalikwa ambao watatoa
mada mbalimbali kuhusu kuinua mchezo wa ngumi Tanzania akiwemo mdau wa
ngumi.Innocente Melleck na mwingine Benedictor Hulilo ambao watakuwa
wageni waalikwa.

Comments