NGASA, KIGI MAKASI WAONGEZWA TIMU YA VIJANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 23

NGASA
KIGI MAKASI
Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwa ajili ya mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroon itakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), Jabir Aziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa (Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar).

Comments