NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO ATEMBELEA DIAMOND JUBILEE

MH.UMMY ALLY MWALIMU AKISAINI KITABU CHA WAGENI KATIKA BANDA LA CARO'S CAKE AMBAO NI MOJA YA WASHIRIKI WA MAONYESHO YA HARUSI TRADE FAIR 2011.
MH.UMMY ALLY MWALIM AKIPATA MAELEZO TOKA MOJA YA MABANDA YANAOYOSHIRIKI MAONYESHO YA HARUSI TRADE FAIR KWENYE UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE JANA
Leo ni siku ya mwisho ya Maonyesho hayo. Wengi wahudhuria kujionea bidhaa, huduma na mapambo ya Harusi. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim, jana alipata muda wa kutembelea maonyesho yanayoendelea ya Harusi ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jana jioni. Akizungumza baada ya kutembelea mabanda yote yanayokadiriwa kuwa zaidi ya 50 ya wajasiriamali tofauti tofauti wanaojihusisha na masuala ya harusi, Naibu waziri alimsifu muaandaaji wa maonyesho hayo, ambae pia ni mbunifu mahiri wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali kuwa ni mjasiriamali anayejituma na ni mfano wa kuigwa. “kwa kweli Mustafa amefanya kitu cha kipekee sana, naa ni mfano wa kuigwa, hii inawapa wafanyabiashara husussani wale wa mapabo na keki kuweza kujitangaza na kujifunza mengi wao kwa wao” alisema mheshimiwa Waziri. Naibu waziri ambae aliweza kupata wasaa wa kubadilishana mawazo na wadau na washiriki wa maonyesho hayo ambao walimpoke kwa furaha huku wakimpa zawadi mbalimbali, aliwasihi na kuwapa moyo wa kuendelea kujituma kwa ari bila kuchoka ili kujipatia kipato na kuwapa huduma wananchi kwa uzuri na usasa zaidi. Nae muaandaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali, ambae ndie aliyekuwa mwenyeji wa mh. Naibu waziri, alisema kuwa maonyesho ya mwaka huu yamekuwa ni ya aina yake kutokana na kujipanga kwa timu nzima ya uandaaji, huku baadhi ya mambo yakiwa yameongezeka tofauti na mwaka jana. “mwaka huu sambamba na maonyesho haya, tumeweza pia kuzindua jarida ambalo ni mahususi kwa masuala ya Harusi, hii ni kwa mara ya kwanza Tanzania kuwa na jarida la namna hii ambalo litatoka mara nne kwa mwaka, pia tumeweza kuwa na midahalo mbalimbali ya wazi ya kuelimisha juu ya masuala ya Harusi na ndoa” alisema Hassanali. Akizungumzia kuhusu muitikio wa watu kuja kutembela maonyesho hayo, Mustafa Hassanali alisema kuwa “kwa mwaka huu, namba ya washiriki imeongezeka zaidi ya ile ya mwaka jana, huku watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya pia inaongezeka siku hadi siku, jana walikuwa wachache, na hii ilitokana na kuwa jana ilikuwa ni siku ya kazi, ila leo kwakweli tumepokea watu wengi sana, na bado tunawaomba watu wajitokeze kwa wingi kwa siku ya kesho ambao ndo tunafunga rasmi maonyesho haya.” Alimalizia kuzungumza Hassanali. Hii ni mara ya pili kwa maonyesho haya ya Harusi kufanyika nchini, huku yakiwa na matarajio ya kuishirikisha mikoa mingi zaidi nchini kwa miaka ijayo, tofauti na mwaka huu ambapo mikoa ya Arusha, Zanzibar na Dar es salaam tu ndio iliyoshiriki.

Kwa maelezo zaidi tembelea http://www.harusitradefair.com/

Comments