MWANAMICHEZO BORA WA TASWA KUONDOKA NA GX 100






MWANAMICHEZO bora atakayetwaa tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) kwa mwaka 2010/2011 atazwadiwa gari aina ya GX 100 yenye thamani ya shilingi mil.13, fedha taslim shilingi milioni moja pamoja na ofa ya kulala usiku mmoja katika hoteli ya Movenipick.


Hayo yalisemwa leo na mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto katika hafla ya kutangaza zawadi iliyofanyika kwenye hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salaam.


Pinto alisema mbali na tuzo hiyo ya jumla, pia mshindi wa kila mchezo atazawadiwa shilingi mil.1, ambapo zaidi ya wanamichezo 35 wa ndani na nje ya nchi watapewa tuzo gizo katika hafla iliyopangwa kufanyika Mei 6 katika hoteli hiyo.

Comments