MO DEWJI, FRIENDS OF SIMBA WAIAHIDI SIMBA MIL.100

MOHAMMED DEWJI 'MO' MBUNGE WA SINGIDA MJINI
BAADHI YA WANACHAMA WA KUNDI LA MARAFIKI WA SIMBA 'FRIENDS OF SIMBA'
MBUNGE Wa Singida Mjini na kundi la Marafiki wa Simba 'Friends of Simba' wameahidi kuipatia kuipatia timu ya Simba kitita cha shilingi mil.100 iwapo itashinda mechi yake na Tp Mazembe kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dewji ambaye ni mfadhili wa zamani wa Simba kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterpriss Tanzania Limited (MeTL) ameahidi kuipatia shilingi milioni 50 huku kundi la marafiki wa Sim,ba nalo likiahidi kiasi kama hicho.

Comments