MIRIAM LUKINDO MAUKI KUZINDUA VIDEO ALBAMU YAKE APRILI 10, DIAMOND JUBILEE

MIRIAM LUKINDO MAUKI MSANII wa muziki wa Injili nchini Miriam Lukindo Mauki anatarajiwa kuzindua video albamu yake ya pili ''NI ASUBUHI' siku ya Aprili 10 kwenye ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Miriam alisema uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo nane unaratibiwa na kampuni ya Haak Neel Production (T) Limited ambapo nyimbo hizo ni pamoja na ‘Ni Asubuhi’ uliobeba jina la albamu, Sema na Moyo Wangu, Anasikia, Amefanya, Wewe ni Sababu, Mungu yu Mwema, Twende na Yesu na Amen Amen. Aidha uzinduzi huo utasindikizwa na Upendo Nkone, msanii wa kimataifa kutoka nchini Kenya Marion Shako, Jackson Bent, Christina Shusho, Whispers Team, Martha Mwaipaja, Upendo Kilahiro, DPC Worship na Living Team.

Comments