MCHAKAMCHAKA MISS KILIMANJARO 2011 WAANZA

GLORY ULOMI, MISS KILIMANJARO 2010. WAANDAAJI wa kumsaka Miss Kilimanjaro kwa mwaka 2011 kampuni ya Edge Entertainment co. ltd wameanza mchakato kabambe wa kusaka warembo bomba ambao wataweza kuuwakilisha vema mkoa huo katika Kanda na hatimaye ngazi ya Taifa. Mratibu wa shindano hilo Methuselah Magese alisema kwamba lerngo la kufanya hivyo nji kuhakikisha wanatoa mrembo bomba ambaye atafanya vema kama si kutwaa taji la Miss Tanzania. Alisema kwa muda mrefu mkoa wao huo wenye historia ya kutoa warembo bora na wenye ushindani mkubwa umeshinda kufurukuta sana katika fainali za Taifa za Miss Tanzania na hasa kushika nafasi tatu za juu. “Tunataka turejeshe hadhi ya mkoa wa Kilimanjaro katika masuala ya urembo, ndiyo maana tumeamua kuingia msituni kusaka warembo bomba ambao tunaamini watakleta changamoto katika mashindano hayo”, Alisema Magese.

Comments