MASHABIKI 600 WA TP MAZEMBE WAJA BONGO KUISHANGILIA TIMU YAO

AMA kweli wenzetu wanazipenda timu zao, kwani mashabiki 600 wa timu ya soka ya Tp watakuja nchini kwa ajili ya kuishangilia timu yao itakapomenyana na Simba jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya ligi ya mabingwa Afrika. Habari kutoka Congo zinasema kuwa mmliki wa timu hiyo Moise Katumbi amefadhili mabasi kumi, lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka kwani kunawengine watakuja kwa usafiri wa njia tofauti. Ili kusonga mbele Simba inahitaji kushinda mabao 2-0, kwani katika mechi ya awali iliyopigwa Lubumbashi Machi 20, Simba ilikwanyuliwa mabao 3-1.

Comments