MAPRO KUTOKA CAMEROON, IVORY COAST, GHANA WAJILETA KUJARIBIWA YANGA



WAKATI timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara zikiwa katika mchakato wa kusaka wachezaji zitakaowatumia katika msimu mpya wa ligi, wachezaji kutoka nchini Cameroon, Ivory Coast, Ghana, Nigeria na Zambia wamejitokeza kuwania kujaribiwa ili wasajiliwe na mabingwa wa ligi hiyo nchini, klabu ya Yanga.
Akithibitisha taarifa hizo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema kwamba wachezaji hao wameshatuma maombi yao, huku wale wa kutoka nchini Nigeria wakiwa tayari wameshatua jijini kwa ajili ya majaribio.

Comments