MAPACHA WATATU, WANAUME TMK JUKWAA MOJA EQUATOR GRILL APRILI 30



KUNDI la muziki wa kizazi kipya Wanaume family TMK watafanya
onesho la pamoja na Bendi ya muziki wa dansi ya Mapacha watatu
Jumamosi ya Aprili 30 kwenye ukumbi wa Aquator Grili Mtoni.
Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa Onesho hilo Zahor Said,
alisema kuwa onesho hilo kwa Wanaume TMK chini ya Said Chege na
Amani Temba watafanya onesho katika ukumbi huo kwa mara ya
kwanza.
Said alisema kuwa katika kunegesha onesho onesho la Mapacha
ameamua kuwashirikisha wana TMK ambao watakuwa maeneo yao.
"Tumeamua kuwapelekea burudani mbili kwa wakati mmoja na siku
moja..wanaume watakuwepo kuwapa tafu Mapacha watatu ambao sasa
nao ni moto wa kuotea mbali"alisema Said.
Alisema onesho hilo litaanza majira ya saa 2 usiku na kufanya vitu vyake
mpaka majogoo.
Bendi hiyo inayoundwa na Wanamuziki Jose Mara, Khalid Chokoraa na
Kalala Junior wana miondoko ya Pangusa Majasho, Chakachua
Twende na Loliondo na mingine mingi.

Comments