KUZIONA U-23 V THE COBS JUMAMOSI BUKU

Mechi ya mchujo ya All Africa Games kati ya timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 (U23) na Uganda (The Kobs) itachezwa Aprili 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya Kijani, Bluu na Rangi ya Chungwa (Orange straight and curve). Kwa upande wa VIP C na B itakuwa

sh. 5,000 wakati sh. 10,000 ni kwa VIP A.

Tunatarajia kuanza kuuza tiketi siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Premier Betting (Kariakoo- Mtaa wa Sukuma, Buguruni Sokoni, Manzese Midizini, JM Mall na Tandale kwa Mtogole), Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Steers (Mtaa wa Ohio na Samora), Big Bon Msimbazi (Kariakoo) na Uwanja wa Uhuru.

UJIO WA UGANDA (THE KOBS)

Timu ya Taifa ya Uganda chini ya umri wa miaka 23 (The Kobs) inatarajia kuwasili

nchini Alhamisi (Aprili 28 mwaka huu) saa 10.30 jioni kwa ndege ya Uganda Air na kurejea nyumbani Jumapili (Mei 1 mwaka huu) saa 11.50 kwa ndege hiyo hiyo.

Msafara wa timu hiyo utaongozwa na Ofisa wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) Sam Lwere na utafikia hoteli ya Durban iliyoko Barabara ya Uhuru, Dar es Salaam.

Timu ya U23 ya Tanzania iko kambini hoteli ya Bamba Beach iliyoko Kigamboni tangu iliporejea kutoka Uganda na inaendelea na mazoezi chini ya Kocha wake Mkuu, Jamhuri Kihwelo.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Comments