KUZIONA TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 23 V CAMEROON BUKU


Viingilio katika mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Cameroon itakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni kuanzia sh. 1,000.


Mashabiki watakaokaa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange) ndiyo watakaolipa sh. 1,000 wakati VIP B na VIP C kiingilio kitakuwa sh. 5,000. Jukwaa la VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa sh. 10,000. Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi.


Tiketi zitauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Bigbon Msimbazi (Kariakoo) na Uwanja wa Uhuru. Mechi itaanza saa 10 kamili. Cameroon imewasili nchini jana saa 5.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikiwa na wachezaji 23 na imefikia Paradise City Hotel. Boniface Wambura Ofisa Habari

Comments