KUMEKUCHA MISS TABATA 2011

CONSOLATA LUCOS, MISS TABATA 2010
Warembo 23 kutoka sehemu mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumtafuta mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2011, ambalo limepangwa kufanyika mwezi ujao. Mratibu wa shindano hilo , Joseph Kapinga, alisema kuwa warembo hao walianza mazoezi tangu Jumapili kwenye ukumbi wa Da West Park, ulioko Tabata. “Warembo wetu tayari wameshaanza kufanya mazoezi pale pale Da’ West Park kila siku kuanzia saa nane mchana," alisema mratibu huyo. Aliongeza kuwa bado kamati ya mashindano hayo inawaomba warembo wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili hatimaye waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala. "Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” Kapinga aliongeza. Kapinga alisema kuwa kampuni yake ya Bob Entertainment ambayo ndiyo inaandaa shindano hilo imepanga kuandaa sherehe maalum ya kuwatambulisha washiriki wote kabla ya kupanga ulingoni kuwania taji hilo . Aliwataja warembo ambao tayari wameshajitokeza kuwa ni pamoja na Marion Augustino (18), Neema Marwa (18), Esther Simon (18), Sweetylily Suleiman (21), Malaika Abdallah (18) na Theckler Benedict (19). Wengine ni Happiness Emmanuel (18), Irene Jafari (19), Janeth Marandu (21), Shadya Ally (21), Victoria Amon (20) na Mgayo Salehe (21). Pia wamo Sarah Hangaya (30), Neema Stanford (21), Upole Athumani (19), Asia Amiri (22), Lucy Paulo (21), Johanita Kanyika (22), Mariamu Lameck (19), Blandina Paul (18), Catherine George (19), Lilian Brayson (24) na Lucia Joseph (20). . Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania . Mrembo anayeshikilia taji hilo ni Consolata Lukosi ambaye katika shindano la ngazi ya taifa mwaka jana alishika nafasi ya tatu na kutwaa taji na la balozi wa Redd's, ' Miss Redds Ambassador'.

Vilevile mwaka juzi Miss Tabata inajivunia kushinda nafasi ya tatu katika shindano la Miss Tanzania kupitia mrembo wake, Julieth William. Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive International.

mwisho.

Comments

Post a Comment