KASEJA, BANKA, MGOSI WATIMULIWA SIMBA

KASEJA, MGOSI NA BANKA KUFUATIA kuukosa ubingwa wa ligi Kuu bara msimu wa 2010/2011 Simba imepanga kuwatimua wachezaji nguli wa timu hiyo wakiwemo kipa Juma Kaseja, Mussa Mgosi, Mohamed Banka pamoja na wachezaji kadhaa. Habari kutoka Simba zinasema uongozi umefikia hatua hiyo kutokana na wachezaji hao kueneza virusi vibaya, kuhujumu, kufitini na kuwagawa wachezaji hali ambayo imechangia timu kufanya vibaya na hasa katika mechi za lala salama na hivyo kuifanya timu kukosa ubingwa kirahisi. Pamoja na hayo, wachezaji hao wamedaiwa kuwa na utovu wa nidhamu uliokithiri kiasi cha kushindwa kuvumilika kwani pamoja na kuonywa mara kwa mara walishindindwa kujirekebisha. Mmoja ya viongozi wa juu wa timu hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini alisema kwamba "hatuwezi kuwarudisha kundini msimu ujao wachezaji hao, wametufanyia mammbo mabaya sana sasa tunataka kuwaonyesha nguvu ya uongozi kwani tuliwabeba vya kutosha", Alisema. "Wamekuwa wakijiona mungu watu, hata kama wana ubora kiasi gani i hatuwez kuvumilia tabia zao mbovu ni bora waende timu nyingine ambapo wanadhani watavumilia upuuzi wao", Aliongeza. Pamoja na hao, wachezaji wengine waliopo katika mkumbuo ni pamoja na Kelvin Yondan, Salum Kanoni na Juma Jabu.

Comments