KANUMBA AMKAMATA NYOTA WA NOLLYWOOD NA KUTOKA NA 'DEVILS KINGDOM'

MSANII WA FILAMU NCHINI STEVEN KANUMBA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU FILAMU YAKE MPYA 'DEVILS KINGDOM' ALIYOMSHIRIKISHA MSANII NYOTA KUTOKA NIGERIA, RAMSEY NOAH (KUSHOTO)
NOAH
KANUMBA
SHAVU MUHIMU NA SISI WANAHABARI

NOAH, SAID MAKALA (CHANNEL 10) KANUMBA

MSANII wa mahiri wa filamu kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah anatarajiwa kuonekana katika filamu mpya iliyotayarisha hapa nchini inayokwenda kwa jina la ‘Devils Kingdom’.

Kanumba alisema kazi ya upigaji picha ambayo imefanywa na kampuni yake ‘Kanumba The Great’ imekamilika, huku ikirekodiwa maeneo ya Kigamboni na katika mji wa Bagamoyo.

“Itakuwa ni filamu ya aina yake ambayo italeta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini...nawaomba mashabiki wakae mkao wa kusubiri mambo mazuri toka katika filamu hiyo”, Alisema.

Naye Noah alisema kupitia ushiriki wake katika filamu hiyo ni sehemu ya mikakati ya ushirikiano baina yake na Kanumba kwani lengo lao ni kufanya mambo makubwa katika tasnia hiyo.

Noah alisema pamoja na kukumbana na changamoto ya kutofautiana lugha na washiriki wenzake,ametumia usanii wake kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama muhusika mkuu.

Mbali na wasanii hao, ndani ya filamu hiyo pia kutakuwa na wasanii wengine akiwemo Patchou Mwamba, Kajala Masanja, Kimlola Kimlola, Stanley Msungu, Bakari Makuka na wengine wengi.

Comments