HARUSI YA PRINCE WILLIAM YATIKISA DUNIA



LONDON, Uingereza

HARUSI kati ya mwanamfalme wa Uingereza, William na mchumba wake Kate Middleton iliyofungwa leo kwenye kanisa la Westminster Abbey, imetikisa nchi hiyo na dunia kwa ujumla.

Wapenzi hao walitambulishwa mume na mke, na Askofu Mkuu wa Canterbury, Rowan Williams mbele ya umati wa watu wapatao 1,900 walioalikwa kuhudhuria kwenye kanisa hilo, huku mamilioni ya watu dunia kote wakifuatilia tukio hilo la kihistoria kupitia runinga.

Tukio hilo ni la kihistoria kutokana na dunia kushindwa kushuhudia harusi ya kifalme kama hiyo kwa muda wa miongo mitatu.

Habari zilisema, katika nchi zenye runinga kubwa mitaani kulionekana umati wa watu wakifuatilia kwa karibu tukio hilo huku wengine wakibubujikwa na machozi kwa kushindwa kuamini kilichotokea kwa wapenzi hao.

Comments