HAPA TMK WANAUME, HA{A MAPACHA 3 NI KESHO NDANI YA EQUATOR GRILL MSIKOSE!

MAPACHA WATATU

BENDI ya muziki wa dansi ya Mapacha Watatu na Kundi la muziki wa kizazi kipya TMK Wanaume Family, kesho watafanya onesho moja kwenye Ukumbi wa Ikweta Grill uliopo Mtoni kwa Azizi Ali, Temeke.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa onesho hilo, Zahor Said alisema kuwa maandalizi ya onesho hilo yamekamilika kama walivyopanga na wapenzi wote wa burudani katika sehemu za Temeke na maeneo ya jirani watarajie mambo makubwa.

Alisema katika onesho hilo litakaloanza saa 3 usiku, watoto wa Temeke, Wanaume Family watakuwa wa kwanza kufanya makamuzi yao juu ya jukwaa ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya onesho kwenye ukumbi huo.

Said alisema mapacha wao watatoa burudani yao ikiwa ni pamoja na kupeleka tuzo zao za Kili Music Awards ambazo walizitwaa kutokana na umahiri wao.

Naye mmoja wa wanamuziki wa Mapacha, Khalid Chuma 'Chokoraa' alisema wanatatoa burudani safi kwa wakazi wa Temeke na vitongoji vyake ambao watafika kwenye ukumbi huo kutokana na kutofanya hivyo tangu kuanza kwa mwaka huu.

"Tuna uhakika wa kufanya mambo makubwa katika usiku huu wa Jumamosi kwa kutoa burudani iliyofanya sisi kupata tuzo ya kili, na hii itakuwa mshangao kwa wakazi wa Temeke," alisema Chokoraa.

Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki watatu ambao ni Chokoraa na Kalala Junior na Jose Mara 'Mtoto wa Kimara'.

Mwisho

Comments