ABDULHALIM HOMOUD:USHAROBARO SASA BASI





KIUNGO mpya wa Azam Fc Abdulhalim Homoud (Pichani)amesema kuanzaia sasa ameachana na mambo ambayo ni kinyume na mafundisho ya dini yake ya kiislam yanavyosema.

Homoud ambaye msimu uliopita alikuwa akikipiga katika klabu ya Simba amesema kuanzia sasa ataachana na mambo ya kujipamba kwa michoro ya ajabu mwilini mwake na badala yake ataelekeza nguvu katika mazoezi na kuswali sala 5.


"Nimeamua kuachana na mambo ya usharobaro kwani nilikuwa nakwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kiislamu, kuanzia sasa ni sala tano na mazoezi", Alisema.

Comments

  1. Brother Abdulhalim,asalaam aleykum
    Natoa pongezi nyingi kwa huo uamuzi ulio chukuwa
    Mnyezi Mungu akujaalie na kukuthibitia hio nia yako.

    ReplyDelete

Post a Comment