ZAWADI KISURA WA TANZANIA ZATANGAZWA




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Zawadi-Kisura wa Tanzania 2010/11KAMPUNI ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), waandaaji wa shindano la uanamitindo la Kisura wa Tanzania, inapenda kutangaza zawadi za washindi wa shindano hilo litakalofikia kilele chake, Machi 18, jijini Dar es Salaam wiki ijayo katika ukumbi wa Kilimanjaro Hoteli.Jumla ya Visura 10 wamefanikiwa kutinga fainali ya shindano hilo, ikiwa ni baada ya mchujo uliofanyika kwa awamu tano, wakiwa kambini katika Hoteli ya Kiromo View Resort, nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, Pwani.Visura waliofanikiwa kutinga fainali na mikoa wanayotoka katika mabano, ni (Glory Msangi-Arusha; Lilian Busa-Mara; Susan Manoko-Dar es Salaam; Joyce Joseph-Dar es Salaam; Neema Seley-Arusha; Flaviana Makungwa-Dodoma; Grace David-Dar es Salaam; Silipa Swai-Mwanza; Letina Christopher-Dar es Salaam na Neema Kilango-Arusha).Visura waliochujwa baada ya kura zilizopigwa na watazamaji wa mchakato wa shindano hilo kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC 1), ni Angel Mombeki na Monica Fikiri wa Tabora (wiki ya kwanza), Asha Hamis na Diana Moshi kutoka Dodoma (wiki ya pili) na Winfrida Sabega kutoka Dar es Salaam na Dotinata Soro wa Arusha (wiki ya tatu). Waliochujwa wiki ya nne, ni Gaudencia Joseph kutoka Mara, Lucy Charles wa Dodoma na Queen Kabisama kutoka Ruvuma, wakati waliochujwa Jumatano wiki hii ni Neema Mathew wa Mwanza, Dorcas Gerald wa Arusha na Rita Swai wa Dar es Salaam.Kwa upande wa zawadi, mshindi wa shindano la Kisura wa Tanzania 2010/11, atapata fedha taslimu Sh milioni 5 pamoja na kuwa Balozi wa FHI kwa mwaka mmoja ambapo atakuwa akilipwa katika kila kazi atakayofanya ya shirika hilo. Zawadi nyingine itakayotolewa katika shindano hilo ni ofa ya kusomeshwa bure kwa mmoja wa Visura hao katika chuo cha mmoja wa wadhamini wa shindano kiitwacho Pure Academy.Pia, wafadhili wetu wakuu FHI watatoa zawadi nyingine tatu za fedha taslimu kwa vikundi vitatu vilivyofanya vizuri katika mpango wa kutoa ujumbe mzuri juu ya elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi, zaidi ikiwa ni janga la ukimwi, kwa wakati wote Visura hao walipokuwa kambini. Zawadi hizo ni Sh milioni 1,400,000 kwa kikundi cha kwanza, wakati kikundi cha pili watapata na Sh 1,050,000, huku kikundi cha tatu kitajizolea Sh 700,000. Vile vile, BTA itatoa ofa ya kumsomesha mrembo mmoja katika chuo chochote kulingana na mapendeleo yake.Visura wote waliofanikiwa kuingia katika kambi ya Kisura wa Tanzania mwaka huu, walipata nafasi ya kufundishwa mambo mbalimbali, zaidi ikiwa ni jinsi ya kujitambua wakiwa kama wasichaan wadogo wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali katika jamii. Pia, Visura hao wamekuwa wakiandaliwa kukabiliana na changamoto tofauti watakazokabiliana nazo, katika nyanja za kiuchumi, afya, kijamii, siasa na nyinginezo. Katika hilo, Visura hao walipata nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwamo kwenda kutembelea na kuwafariji wahanga wa mabomu yaliyolipuka katika kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) iliyopo Gongolamboto, Dar es Salaam, waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Amana, jijini. Waliweza pia kutembelea vituo vya watoto yatima Bagamoyo na Dar es Salaam.Visura hao pia walifanya ziara katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, jijini, ambako walijionea utendaji wa shughuli mbalimbali uwanjani hapo. Walitembelea pia SBC limited ili kuona ni jinsi gani kinywaji cha Mirinda kinategenezwa. Leo wanatembelea TBL ili visura waweze kujifunza ni jinsi gani kinywaji REDDS kinategenezwa.Pamoja na kuwa shindano hilo linahusu kumtafuta mwanamitindo (model) ambaye atafanya shughuli zake ndani na nje ya nchi, malengo makuu ya shindano la Kisura wa Tanzania ni kuwajengea uwezo watoto wa kike kwenye kiwango cha uelewa na kujitambua katika mabadiliko ya tabia, kwa kuwapa elimu iliyopo katika mfumo rasmi (shuleni) na ile iliyopo nje ya mfumo rasmi.Vile vile, shindano hilo linalenga kuwafundisha Visura masuala ya uzazi, afya pamoja na jinsi ya kujikinga na magonjwa hasa ugonjwa wa ukimwi. Kuwafundisha wasichana hao ujasiriamali ili waweze kuwa vinara wa mabadiliko katika maisha yao na kwa taifa zima kwa ujumla na kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye. Shindano la Kisura wa Tanzania, linawatumia wanamitindo kama nyenzo ya kuelimisha na kufikisha ujumbe kwa jamii ya kitanzania. Kisura wa Tanzania 2011 imeandaliwa na BTA na Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBL kwa kupitia kinywaji chake cha REDDS, TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL, MJ Records, I-View Media, PURE Hair and Beauty Spa na PURE Academy of Aesthetics.

Comments