YANGA KUTEUA MRITHI WA MOSHA APRILI 3

DAVIES MOSHA
Kamati ya Utendaji ya klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kukutana Aprili 3 kwa ajili ya kuteua jina la mjumbe atakachukua nafasi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Davies Mosha.
Hatua hiyo inatokana na Mosha kujiuzulu hivi karibuni kwa madai ya kutukanwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo,hivyio kujiweka kando ili kulinda heshima na usalama wake.Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga amesema maamuzi hayo yametolewa katika kikao cha kamati ya Utendaji kilichokutana jana na kujadili hatua ya kujiuzulu kwa Mosha pamoja na mambo mengine.
Kabla ya Mosha, viongozi wengine waliojiuzulu chini ya uongozi wa Nchunga ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Lawrence Mwalusako, Kocha Mserbia Kostadin Papic, Meneja Emmanuel Mpangala na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Seif Mohammed.

Comments