WAZIRI NCHIMBI KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA TFF KESHO

RAIS WA TFF, LEODGER TENGA
Mkutano Mkuu wa mwaka 2010 wa TFF unaanza Machi 26 mwaka huu ukumbi wa NSSF
Water Front, Dar es Salaam.
-Mkutano huo utakaoanza saa 3 kamili asubuhi utafunguliwa na Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi.
-Mkutano huo utakaokuwa na ajenda 16 utamalizika Machi 27 mwaka huu.
-Wajumbe wa mkutano ambao wamefikia hoteli za Valentino iliyoko Mtaa wa Aggrey
na Spice Inn, Mtaa wa Lumumba.
-Ajenda za mkutano ni;
Kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kusoma na
kuthibitisha ajenda, kuthibitisha muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu uliopita,
Yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za
utekelezaji za wanachama, kupitisha taarifa za utekelezaji wa Kamati ya
Utendaji, kupitisha taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka uliopita, kupitisha
taarifa ya wakaguzi na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2011,
uchaguzi wa nafasi zilizo wazi, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba
ya TFF (kujadili mikoa mipya), kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na
wanachama au Kamati ya Utendaji, Mengineyo na Kufunga kikao.
Boniface Wambura
Media Officer TFF

Comments