WANACHAMA WAMREJESHA YANGA DAVIS MOSHA

MOSHA AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA MAKAO MAKUU YA KLABU YA YANGA
MOSHA AKIWA MEZA KUU NA BAADHI YA WANACHAMA
MOSHA AKIINGIA KLABUNI

MMOJA YA WANACHAMA WA YANGA

WANACHAMA WAKIMSIHI MOSHA KUBADILI UAMUAZI
MOJA YA BASI LILILOWABEBA WANACHAMA HAO
BAADHI YA WANACHAMA WALIOSHUKA KATIKA MAGARI NA KWENDA NYUMBANI KWA MOSHA

WANACHAMA wa klabu ya soka ya Yanga wamefanikiwa kumrejesha madarakani makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha ambaye hivi karibuni alijiuzulu kutokana na sababu mbalimbali. Wanachama toka matawi 11 ya jijini Dar es Salaam na Pwani waliandamana hadi nyumbani kwa Mosha ili kumshinikiza arejee kuingoza Yanga wakidai kuwa ndiye kiongozi mwenye uwezo wa kuiongoza klabu hiyo. Wakiwa katika msururu wa magari aina ya Coaster nne, hiace 2, bajaji na magari binafsi wanachama hao waliwasili nyumbani kwa Mosha Mikocheni na baada ya kuzungumza naye kwa kina kabla kumtaka kwenda klabuni kwa ajili ya kuzungumzia mustakabali wake. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanachama hao walisema wameona Yanga inayumba baada ya kujiuzulu kwake, hivyo hana budi kurejea ili kuinusuru klabu hiyo. Wakienda mbali zaidi, wanachama hao walidai kuwa licha ya mwenyekiti wao Lloyd Nchunga kudai hawezi kufanya kazi pamoja na Mosha,inaonyesha wazi kuwa ndiye chanzo cha msigano baina yao na ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu alizokuwa kifanyiwa Mosha.

Comments