TUPO WACHEZAJI WENGI NCHINI, NI BORA NA WENGINE KUITUMIKIA STARS-JERRY TEGETE


SIKU moja baada ya kutangazwa kwa kikosi cha timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ huku baadhi ya wachezaji mahiri wakitemwa, mmoja ya wachezaji waliotemwa Jerry Tegete amesema ni wakati wa wengine kujaribu.
Tegete amesema haoni vibaya kutoitwa katika kikosi hicho kwani kwa sasa Tanzania ina wachezaji wengi wazuri ambao nao wanastahili kuwemo katika kikosi hicho.
Alisema, kocha kama mtaalamu wa soka anamaamuzi yake katika kuchangua wachezaji ambao anaona wanastahili kuwemo jatika kikosi hicho na kucheza kwa mafanikio zaidi.
Mshambuliaji huyo wa Yanga aliongeza kuwa, kwa hali hiyo ndiyo maana kocha wa Stars, Jan Poulsen amekuwa akibadili wachezaji katika kikosi chake kila mara na hasa wale waliozoeleka kuwemo akiwa na malengo yake.
“mimi sidhani kama kuna ubaya wowote wa mimi kutokuwemo katiak kikosi cha Poulsen, kwa sasa Tanzania kuna wachezaji wengi na wazuri sana hivyo inabidi kila mmopja apate nafasi ya kuingia kundini”, Alisema.
Hata hivyo, Tegete alipinga madai ya kuwa na kiwango kidogo hali ilioyopelekea kuenguliwa katika kikosi hicho ambacho kinajiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Afrika Kati, akisema kuwa yupo katika hali nzuri kama ilivyo zamani.
Tangu Poulsen kuaza kuinoa Stars amekunywa akiwaita na kuwatoa wachezaji mahiri ambao wamekuwa hawakosekani katika kikosi hicho tangu kuibuka kwao katika medani ya soka akiwemo pia mshambuliai wa Simba, Mussa hassan Mgosi.

Comments

  1. Nafikiri ni vyema tukamuachia kwanza kocha akafanya vitu vyake, maana Watanzania tunapenda sana mpira wa mdomoni!

    ReplyDelete

Post a Comment