TP MAZEMBE KUWASILI IJUMAA, KIINGILIO CHAO NA SIMBA SHILINGI 5,000

OFISA HABARI WA SIMBA, CLIFFORD NDIMBO
MABINGWA wa soka barani Afrika TP Mazembe ya Congo wanatarajiwa kuwasili ijumaa tayari kwa mechi yao ya marudiano na Simba itakayopigwa jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ofisa habari wa Simba Clifford Ndimbo ametaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni :

Sh.40,000 (VIP A), sh.20,000 (VIP B), sh.10,000 (VIP C), sh.8,000 (VITI VYA ORANGE), sh.5,000 (VITI VYA KIJANI NA BLUU).

Tiketi zitauzwa katika vituo vifuatavyo:MIGAHAWA YA STEERS, VITUO VYA MAFUTA VYA BIG BON, JENGO LA BENJAMIN MKAPA, BP MWEMBECHAI NA UWANJA WA TAIFA.

Comments